Thread Reader
Rasheed Mfaume Umary

Rasheed Mfaume Umary
@CheedKhalifa26

Mar 16
23 tweets
Twitter

HISTORIA NA VITUKO VYA BI KIDUDE “Mie naimba kwa kutumia kichwa, si kifua au kubana pua aaa! Sifanyi kama hao wanaojiita waimba taarabu wa siku hizi, kwanza siku hizi hakuna taarabu. Mimi nina uwezo wa kuimba bila kutumia karatasi kwani bendi ya polisi...✍️👇 #MuzikiNiMaisha

(kicheko kwa wanaomsikiliza). “Enzi zetu taarabu ulikuwa mtu ukiisikiliza ufanye kazi kupata maana yake “Taarabu ya zamani mtu ulikuwa ukitikisa kichwa taratibu, wanawake tulikuwa tunavaa kwa heshima, si siku hizi watu mnakatika mabuno (viuno),
wanawake wanakwenda bila heshima, au kwa vile kuna matako ya Kichina?” alihoji mwanamuziki huyo huku akitoa pakiti yake ya sigara aina ya Embassy na kuvuta. Kuhusu sigara na uimbaji, Bi kidude alikuwa hakubaliani na dhana kwamba inamaliza sauti, badala yake alitoa shuhuda
wamba ameanza kuvuta akiwa kijana lakini sauti yake haina mabadiliko. “Nimevuta sigara mie hujazaliwa na mpaka sasa navuta sijapata TB wala ugonjwa wa mapafu, leo unaniambia mbaya! Mbona sijafa?” alihoji mkongwe huyo na kueleza kwamba alianza kuvuta
sigara aina ya Seven Seven, Mkasi, Simba, Kulindondo, Gundufleki na ya mwisho ilikuwa Embassy ambapo alikuwa ana uwezo wa kumaliza pakiti moja kwa siku tatu.
Mbali ya kuimba, pia Bi kidude alikuwa ana uwezo wa kupiga ngoma, ikiwa ni baada ya kujifunza kwenye majahazi wakati akiwa na umri mdogo alipokuwa akitoroka kwenda madrasa (chuo cha elimu ya Kiislamu). “Nilikuwa nakimbia nyumbani, naaga naenda chuo lakini sifiki,
nazuga kwa kubeba juzuu yangu kwapani lakini siendi huko, bali nakwenda kwenye majahazi kufundishwa kupiga ngoma na tumba,” alisisitiza.
Oktoba mwaka 2005 alipata Tuzo ya heshima ya msanii mwenye mafanikio makubwa iliyotolewa nchini Uingereza (Tuzo ya WOMAX). Aliyebaini kipaji chake Bi Kidude, anapasua ukweli kwamba mtu wa kwanza kuthamini kazi zake na kumtafuta hadi kufika alipo alikuwa
Rais Mstaafu wa Tanzania wa Awamu wa Pili, Ali Hassan Mwinyi Anasema alipokuwa Rais wa Zanzibar, aliwaomba watu wamtafute Bi Kidude ili apate kumwimbia nyimbo za Siti, kwa kuwa hakuna aliyeweza kuziba pengo japo kidogo la Siti binti Saad.
Anasema alipokuwa Rais wa Zanzibar, aliwaomba watu wamtafute Bi Kidude ili apate kumwimbia nyimbo za Siti, kwa kuwa hakuna aliyeweza kuziba pengo japo kidogo la Siti binti Saad.
“Ali Mwinyi alikuwa akitafuta nyimbo za Siti binti Saad. Aidha, anafahamisha kwamba alipelekwa kwa mara ya kwanza nchini Ujerumani na Mariam Hamdani, (dada wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakhia Hamdani Meghji) alikuwa anakuja kunipiga picha anapeleka Ujerumani miye Bi Kidude
Ndie aliyemtambulisha kwa watu mbalimbali ambapo aliweza kusimama kwenye majukwaa na kutumbuiza. Kama hiyo haitoshi, Bi kidude aliongeza kwa kusema Mariam alimpeleka hadi kwa Malkia Elizabeth II nchini Uingereza.
“Yeye ndiye alinipeleka Ulaya, sikujua Kiingereza, nikawa na mlinzi, miye nimefika hadi kwa Malkia Mtukufu Lizabet (Elizabeth)... akawa ananisalimia Shikamoo mama Kidude.
“Nimepewa cheo na Mtukufu Lizabet. Nilipofika anafunua vitabu naona sura yangu nikawa nashangaa, alinipa kidani cha dhahabu nikaamua kukiuza kulekule Uingereza, maana ningekuja nacho huku wangeniua,” alisema.
“Nimepewa cheo na Mtukufu Lizabet. Nilipofika anafunua vitabu naona sura yangu nikawa nashangaa, alinipa kidani cha dhahabu nikaamua kukiuza kulekule Uingereza, maana ningekuja nacho huku wangeniua,” alisema.
Katika hilo, Bi kidude alisema alipofika kwenye kasri la malkia alikutana na askari waliofanana na sanamu, wamevalia viatu vya chuma huku akieleza kwamba hajawahi kuliona kochi kama aliloliona huko.
“Wakati natoka kwa Mtukufu Lizabet nilijikojolea ndani ya gari kwa hofu mambo niliyoyaona makubwa,” alisema Bi Kidude ambaye ni binamu wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Salmin Amour.
Akiwa nje ya Tanzania, mkongwe huyo alieleza alivyothaminiwa huku akisisitiza kwamba Mkurugenzi wa Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), Ruge Mutahaba, pia alimsaidia na kumfikisha alipofika.
“Mimi, Ruge miye sikumjua huku, kanikuta napiga ngoma kwa Shakira, kanipenda akanichukua kaenda kunikodia hoteli alipojua naimba ndo akanikaribisha ofisini kwake, tunaongea ananihoji, kisha ananipa pesa anaondoka, mie nabaki hotelini tena.
“Siwi na shida miye, nakwenda ofisini kwa Ruge, simuombi mwenyewe ananigawia pesa, ananiuliza upo au haupo, namwambia narudi Unguja na yeye akija Unguja lazima afike nyumbani kwangu, anachukua alichonacho ananigawia, simuombi aah! Ananitumikia yeye mwenyewe.
Bi Kidude alfariki 17 Aprili 2013,uko Bubu Zanzibar. Apumzike Salama Mkongwe wa Muziki wa Taarab.🙏🕊️
NB: Tuongeeni serious nipeni Gigs Kijana wenu niendelee Kuupiga Mwingi.🙏 Kwenye BIO kuna link ya namba yangu itakuleta WhatsApp kwa Gigs/ Pia unaweza kuongeza kama Idadi ya Washikaji zako nitext nikuSave.🤜🤛
Asante kwa kuwa na Mimi RT LIKE COMMENT FOLLOW MIMI Tuendelee kuwa Pamoja kwenye Makala Mbalimbali.🙏
Rasheed Mfaume Umary

Rasheed Mfaume Umary

@CheedKhalifa26
Youth Entrepreneur/Youth Motivational Speaker/A Fun Guy/GGMU💖/YANGA🔰/Social Media Lover/Entertainment Lover/Thread Writer🧵⌨️...A Smarter Youth in a Global.
Follow on Twitter
Missing some tweets in this thread? Or failed to load images or videos? You can try to .