Thread Reader
Fortunatus Buyobe

Fortunatus Buyobe
@fbuyobe

Nov 24, 2022
11 tweets
Twitter

John Kunambi anahitimu stashaada ya Uandishi wa habari. Nje ya taaluma yake, John anavutiwa sana na upigaji wa picha za mjongeo (video) na mnato (still picture) Mjomba wake aishiye Uingereza anamsuprise kwa kumnunulia kamera kali kabisa ya kisasa. NYOKA (CODE & DECODE) UZI👇

John akapata ajira katika kampuni iliyokuwa inamiliki gazeti la habari za uchunguzi. Mmiliki wa gazeti lile alikuwa haishiwi misukosuko ambayo kuna nyakati iliishia kumlaza korokoroni kutokana na habari za gazeti lake kugusa wanasiasa wenye nguvu kisiwani.
Ilikuwa ni swala la kawaida kwa polisi wa kisiwa kuvamia chumba cha uchapaji kuzuia habari flani isichapishwe baada ya taarifa fiche kubaini kuna kigogo ataguswa. Uvamizi huu ungeishia na kuondoka na mmiliki na kupewa kashkashi. Lakini mmiliki huyu hakukata tamaa.
Kuna wakati mmiliki huyu aligombana nyoka wa mdimu. Kilichofata ilikuwa ni kuvamiwa kwa mmiliki akiwa anarudi kiotani kwake na kujikuta anang’olewa jicho na kucha. Turudi kwa John, Sasa John akawa naye ni mwajiriwa kwenye this controversial newspaper. Akiwa mwandishi bora
Ukiachana na kazi hii ya uandishi John alikuwa akiitumia kamera yake kutafuta matukio ya udaku mitaani na kisha kuuza picha kwenye magazeti ya udaku. Kazi hii ilimpatia kipato kizuri zaidi hata ya mwajiri wake ramsi. Ndipo ikatokea siku moja jioni katika ufukwe wa mikoko.
Ilikuwa ni katikati ya kampeni za uchaguzi mkuu wa kisiwa mwaka ule. John akiwa mehaa vya kutosha kusaka udaku bila mafanikio. Majira ya kama saa mbili usiku yalimkuta john akitembea pembezoni ya bahari akiwa katika harakati za kuondoka kwa kukata tamaa.
Mara akaona tukio moja la ajabu sana. Aliona wanausalama wakiwa wanasukuma gari aina ya shangingi likiwa na namba za sebuleni kabisa. Ndani ya gari aliona mtu aliyekuwa anafahamika kabisa akiwa kaegemea usukani. Tukio likamfanya John akumbuke kamera yake yenye night vision
John akaanza kutwanga mapicha akiwa kajificha maeneo. Akawa anazoom anachukua picha mjongeo na mnato. Aliyafanya yote haya hata bila kuwajua kama ni anapiga picha udaku au lah! Kifupi alipiga picha zile bila sababu Kesho yake ndipo alijua amepiga picha za kifo.
John hakujua kama Mmiliki wa gazeti ile pamoja na misukosuko aliyokuwa anaipata alikuwa ni undercover. Yeye aliona huyu ndio mtu ambaye anafaa kushirikisha jambo lile hasa baada ya msiba wa kitaifa uliofatia kesho yake. Marehemu akisemwa amekufa kwa ajari. Gari iliyosukumwa.
Umeshawahi kujua linalotokea endapo unataka kujua mbwa ana meno mangapi huku mbwa naye anataka kujua binadamu ana vidole vingapi?
Sogelea telegram link👇 t.me/fbuyobe
Fortunatus Buyobe
Pool of thoughts. A commander of the hand to mouth battalion. Environmental Pioneer. Social Engineer. #CertifiedMchapaUzi . Telegram: https://t.co/aEEOOryJWO
Follow on Twitter
Missing some tweets in this thread? Or failed to load images or videos? You can try to .