Thread Reader
Boniface Jacob

Boniface Jacob
@ExMayorUbungo

Mar 3, 2023
66 tweets
Twitter

SOMA UZI MPYA HAPA.......πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡ UNTOLD STORY/RELEASED 4th MARCH/UNCLASSIFIED LEO NI 4 MARCH MWAKA MMOJA tangu MBOWE atoke GEREZANI baada ya KUFUTIWA KESI..! KWA NINI MBOWE ALISHITAKIWA KWA UGAIDI NA KWA NINI MBOWE ALITOLEWA GEREZANI 4 MARCH.!

Ilikiwa Jumatano ya tarehe 17 March 2021 Mida ya Saa 1 Usiku Kwenda Saa 3 usiku.ambapo Makamu wa Rais wa JMT alitamgazia Dunia kuwa Rais John Pombe Magufuli ameaga Dunia (amefariki) Muda wa Saa 12 Jion ktk Hospitali ya Mzena,Kijitonyama na Chanzo Cha Kifo ni maradhi ya Moyo.
Tarehe 19 March 2021 siku 4 baada ya Kututangazia Kifo cha Dk.John John Pombe Magufuli Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Hassan Suluhu alikula Kiapo cha Kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Samia Hassan Suluhu akatutangazia ratiba ya Mazishi na Kuongoza mazishi
Tarehe 26 March 2021 Rais John Pombe Magufuli alizikwa Kijini kwao,Milimani,Wilayani Chato Mkoa wa Geita katika makaburi ya familia
Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema ambaye wakati wa Msiba Rais Magufuli hakuwepo Tanzania Alikuwa akiishi Dubai na muda mwingi Nairobi,Kenya Aliporejea Tanzania alifanya mkutano wa Waandishi wa habari na Kutoa hotuba ya "NEVER AND NEVER AGAIN" Umagufuli usijirudie tena....!
Hotuba ya Freeman Mbowe ya Tarehe 11 April 2021 ya "NEVER AND NEVER AGAIN" ilipokelewa kwa hisia tofauti ktk kila Sehemu na Kwa Wananchi Wapo walioisifia Wapo walio ipenda Wapo iliyo wakwaza Wapo iliyo wagusa mioyo Lakini Serikalini kwa Vyombo vya Dola ilikuwa ni fedhea kubwa
Basi Bhanaaaaa Wakati Watu wote Wanajiweka sawa kutafuta nafasi katika serikali Mpya ya awamu ya Sita ndani ya Serikali na ndani ya Vyombo Vya Dola Hotuba ya Mbowe ya Never and Never again ilikuwa Mwiba Sana Kwa Wengi waliokuwa Watawala na Viongozi wa awamu ya tano
Kila mmoja alijipa nafasi ya Kujiweka Karibu na Kuonyesha umuhimu wake kwa nahodha mpya Samia Suluhu wa Jahazi letu la JMT Hapo ndipo Kila Mmoja akawa Karibu Kushauri na Kushawishi umuhimu wake. Na Kila mmoja anakwepa kuonekana alishiriki kuumiza na Kukandamiza watu awamu ya 5
Tarehe 28 June Mwaka 2021 kama Mwelekeo mpya wa awamu ya Sita ulimuachia Kamanda wa Chadema Mdude Nyagali Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya. Kama alama ya Mwelekeo Mpya wa Siasa za awamu ya Sita, Wakati huo Bavicha waliamua kubeba ajenda ya Katiba Mpya kwa nguvu kubwa sana
Siku ya Alhamis ya tarehe 01 Mwezi July 2021 Siku tatu yoka atoke gerezani Mdude Nyagali alikuwa miongoni mwa Wageni waliofika katika Kongamano la Vijana pale Segerea ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbowe Ktk kongamano lile Mdude alitoa msimamo wa Kiharakati wa kutoweka Silaha Chini
Basi Bhanaa baada ya Kongamano lile tuh Wakuu wa Vyombo vya Dola wote Kwa Pamoja katika kutafuta Uhakika na nafasi zao Wakaomba kazi ya kusaidia Kudhibiti Upinzani kama awamu ya tano huku wakitabiri Rais Samia atashindwa kutawala endapo Wapinzani tutakuwa huru kuendelea na siasa
Wakati Bavicha Wanatangaza Kupeleka Kongamano la Katiba mpya Mwanza Tatehe 31 July 2021 Kumbe walikuwa wanathibitisha fitina za vyombo vya Dola kwamba "Nchi haitotawalika,Wataenda Kila sehemu kukutukana,Hawakuheshimu sababu wewe ni Mwanamke " USIWACHEKEE Na Rais akawasikiliza
Matokeo ya Rais Samia Kukubaliana na Vyombo vya Dola juu ta Kudhibiti Wapinzani kama ilivyokuwa awamu 5 Jeshi la Polisi Ilemela Kwa Kupokea maagizo Kutoka Juu lilipiga Marufuku Kongamano la Bavicha la tarehe 21 July 2021 Kuhusu Katiba Mpya Kwa Barua ya Polisi ya 16.07.2021
Wakati Jeshi la Polisi linazuia Kongamano la Bavicha la Katiba Mpya Jijini Mwanza tarehe 16 July 2021 Mwenyekiti F.Mbowe alikuwa Msibani Moshi wiki hiyo Kwa Maombolezo ya Kifo cha Kaka yake Charles Mbowe kilichotokea 09 July 2021 hospitali ya KCMC,Moshi Akaona Katazo la Polisi
Mwenyekiti F.Mbowe baada ya Mazishi ya Kaka yake tuh alipaa na kutua Jijini Mwanza tarehe 19 July 2021 Siku 2 kabla ya Kongamano la Katiba mpya na Kutangazia Waandihi wa Habari mkoni Mwanza "KONGAMANO LIPO PALEPLE" anasema alisukumwa na Hotuba yake ya "NEVER AND NEVER AGAIN"
Siku ya Kongamano la Tarehe 21 July 2021 Alfajiri na Mapema sana Jeshi la Polisi lilizingira Hotel ya KINGDOM ya Jijini Mwanza waliyofikia Viongozi wa Chadema na Kufungua Kila Chumba Alikamatwa F.Mbowe wenzie 10 wakapelekwa kituo cha kati Isipokuwa Mbowe wakampeleka Mafichoni
Habari za Kuulizia alipo Mbowe zikawa Kubwa zikaenea Nchi nzima 22 July 2021 Jeshi la Polisi Kutipia Kamanda SACP Ramadhan Ngh'anzi wa Mkoa wa Mwanza akaithibitishia Dunia kuwa "Jeshi la Polisi linamshikikia Mbowe kwa Tuhuma za Ugaidi na Mauaji ya Viongozi wa Serikali" πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Siku ileile ya Tarehe 21 July 2021 Jeshi la Polisi walikuwa wameshamfikisha Freeman Mbowe Dar es Salaam Na Saa 5 hadi Saa 9 za Usiku Walifanya Upekuzi nyumbani kwake Mikocheni Zoezi la Upekuzi lilikuwa linasimamiwa na DCP Ramadhani kingai na Makachero wengine wa Polisi
Mwenyekiti F.Mbowe anasema Wakati wanapekua Nyumbani kwake Mikocheni DCP Ramadhan Kingai alimwambia "Umetusumbua Sana,Safari hii Utoki,Tunakupa Kesi ya Ugaidi" Maneno ambayo Wakili John Malya aliyekuwa nje ya Nyumba Wakati wa Upekuzi wa nyumba ya Mbowe anayaunga Mkono.
Bada ya upekuzi wa Usiku wa tarehe 21 July Kuamkia tatehe 22 July Huku Jeshi la Mawakili mbalimbali likijisajili kutaka Kusimamia Kesi ya Mbowe Zikapita Siku 3 Mbowe akiwa mikononi Mwa Jeshi la Polisi bila kupelekwa Mahakamani Familia yuh ndiyo waliruhusiwa kupeleka Chakula
Mawakili wa Chadema pamoja na Mawakili Wengine Wakakimbilia Mahakama Kuu kutaka Mahakama itoe "HABEAS CORPUS" Polisi Wamuachie huru Freeman Mbowe au Wamfilishe Mahakamani haraka sana Huku nyuma yake Polisi wakampeleka Mbowe Mahakamani Kinyemela bila Mtu yoyote Kujua wala Wakili
Ilikuwa hiviiiii Familia ya Mbowe ilipeleka chakula cha Mchana kama Kawaida kwa sababu hata Mawakili hawakuruhusiwa kuonana Mbowe Mke na Watoto wa Mbowe walipopeleka Chakula Kituo cha Polisi Oysterbay Siku hiyo utaratibu wakapewa tofauti,Wakaambiwa wakiache wao polisi watampa
Lakini Katika kila Kundi la Polisi wakayili lazima awepo Mmoja mwema na Mchamungu Polisi Mmoja Oysterbay aliona familia ya Mbowe wakipewa Maelezo Akatoka zake akaenda nje ya Kituo kama anaendelea na Kazi zake Akapishana nao wakiwa wanaondoka akawatonya "MBOWE HAYUPO HAPA"
Ndipo famili ikarudi nfani na Kulazimisha kutaka Kumuona Ndugu yao Kwanza Wakadanganywa na Viongozi wa Polisi kuwa Mbowe amejisikia Vibaya kapelekwa Hospitali Walipokuwa wagumu Kuelewa wakaambiwa Mbowe kashapelekwa Mahakamani Mawakili Wakakimbilia Mahakamani wakakuta HEWAAAA
MBOWE ALIKUWA TAYARI AMESOMEWA MASHITAKA YAKE HARAKA SANA NA KWA SIRI SIKU YA TAREHE 26 JULY 2021 NA KUPELEKWA GEREZA LA SEGEREA Chadema Wakatoa taarifa hiyo ya Kusikitisha kwa Umma Majira ya Saa 10 Jioni siku ya 26 July 2021
Basi Bhanaaa Tarehe 26 July 2021 ndiyo ikawa siku ya Kwanza ya Usajili wa Mbowe kutoka Uraiani kwenda Kulala Jela. Wakuu wa Vyombo vya Dola walishangilia Sana kwa Sababu 1.Wamemfundisha Kwa Vitendo Mbowe kuwa "NEVER SAY NEVER" 2.Walifanikiwa kuonyesha shida siyo Rais Magufuli
Wakishangilia na Kupiga Mvinyo wa furaha kwa Kufanikiwa hatua ya Kwanza walibakia na Mitihani mikubwa 3 kwa Rais 1.Kuhakikisha kufungwa Mbowe hakuleti Madhara Nchini 2.kuhakikisha Mipango yote inakaa Sawa Kumtia hatiani Mbowe 3.Wanakabiliana na Presha za ndani na nje ya Nchi
Wakati huo wote Dunia inasubiri Kwa hamu kuona hati ya Mashitaka anayokabiliwa nayo Mbowe Na Sababu za Msingi za Serikali kumuweka kizuizini Mbowe Na kama Ugaidi na Mauaji yapo ya Viongozi anayohusika nayo Chadema walihamasishana kwa ajili ya Tarehe 05 August 2021 kuja Kisutu
Kwa Mujibu wa Sheria zetu Mahakama ya Kisutu haikuwa na Uwezo wa Kusikiliza shauri la Ugaidi na Mauaji anayo tuhumiwa Mbowe Siku ya 26 July 2021 Mbowe alifikishwa Mahakama ya Kisutu ila hakutakiwa Kusema lolote mbele ya Hakimu Mkazi Badaka yake Kesi iliitwa tarehe 5 August 2021
Jeshi la Polisi lilijua fika kwakuwa kesi imeirwa Tarehe 05 August 2021 watu wangejaa kutaka Kumuona Mbowe na Kushuhudia Kesi yake Mahakama ya Kisutu Basi IGP Simon Sirro akajitokeza ktk Vyombo vya Habari kuwatisha Watu wasije Kisutu na Kwamba atakaye Kuja atakutana na Chamoto
Ikawa ni Wiki ya moto sana kutoka Tarehe 26 July 2021 hadi tarehe 5 August 2021 siku ya kesi kuitwa Polisi waliendesha msako Dar es Salaam nzima kuwinda Viongozi wa Chadema Makachero wa Polisi walipangwa kila ofisi za Chadema zilipo ndani ya Dar es Salaam Kamata kamata ikaanza
Katika Msako wa Jeshi la Polisi na kamata kamata mpaka tarehe 01 August 2021 walikuwa wamekamata viongozi kadhaa wa chadema Kwa kuhusiwa kuhamasisha Wanachama na wananchi kufika kwa wingi Mahakama ya kisutu
Siku moja kabla ya kesi,Siku ya J,tano ya tarehe 4 August 2021 Viongozi wa Chadema wafuatao walikuwa wamekamatwa 1.julius Mwita 2.Gervas Lyenda 3.Alex Massaba 4.Omar Mkama 5.Aisha Machano 6.Fatma Tabith 7.Patrick Asenga 9.Jacob Bailemba 10.Deogeatius Kajula 11.Abdalah Senkamba
Katika Kamata kamata hii Mimi hawakunipata kabisaaaa Nilikuwa Bar ya Mtaani nikaona Makachero wa Polisi wamefika na Kuomba Meza na Wao Nikaacha Chakula na Kinywaji nikajifanya naongea na Simu nikatokomea Vichochoroni Kisha nikatuma Mtu aifuate gari yangu Nikawaaacha peke yao
Siku ya Kesi sasa Tarehe 05 August 2021 siku ya Alhamisi la Polisi lilizingira Mahakama yote ya Kisutu tangu Alfajiri na Kuweka Ulinzi Mkali ikiwemo Doria za Kuzunguka mitaa Yote ya Kisutu
Wafuasi wa Chadema na Wao hawakuogopa Kitu mbele ya Mwenyekiti wao Freeman Mbowe Dhidi ya mashitaka mazito ya Kushtua ya Ugaidi na Kuua Viongozi wa Serikali
Tarehe 05 August 2021 pamoja na Watu wengi Kujaa ndani na nje Mahakama ya Kisutu ya Mahakama Magereza hawakumfikisha Freeman Mbowe Mahakamani siku hiyo Walitaka Kuendesha Kesi kwa njia ya Video,Mbowe asomewe Mashitaka Yake akiwa Gerezani Segerea Video ya Mahakama ikawa Mbovu
Mahakama baada ya Kuona Tekinolojia imeshindikana kwa Kumsomea Mashitaka yake Mbowe akiwa Gerezani alafu Hakimu na Mawakili wakiwa Kisutu Hakimu aliagiza Mbowe aletwe Siku inayofuatia Ya Ijumaa ya Tarehe 6 August 2021 Saa 3 Asubuhi Wafuasi wengi wa Chadema Walikamatwa siku hiyo
Kwa mara ya Kwanza Sasa Mbowe akaonekana Asubuhi siku ya Ijumaa ya tarehe 06 August 2021 Ktk Mahakama ya Kisutu tangu akamatwe 21 July 2021 Akashushwa mlango wa Nyuma akiwa katika Kibasi Kidogo na Wenzie akina Khalifan Bwire,Adam Kasekwa na Mohammed Ling'wenya
Tarehe 06 August 2021 ltk Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu Kesi ya Mbowe na Wenzake Walisomewa Mashitaka Upya bila Kutakiwa Kujibu Chochote Ilihairishwa hadi 13 August baada ya Serikali kusema haijamaliza taratibu za Kuandaa Nyaraka za Kuhamishia Kesi hiyo Mahakama yenye mamlaka
Dunia ikiwa inasubiri tarehe 13 August 2021 hatima ya Kesi ya Mbowe Watu wa Usalama Wakamtengenezea Inteview Rais Samia ikiwa katikati ajibu tuhuma za Serikali yake Kumbambikia Kesi Mbowe Hapa Watu wa Mfumo na Dola waliharibu Vibaya Sana taswira ya Rais Ingawa kwao ni ushindi
Katika Mahojiano yale Watu wa Mfumo na Dola walifanikiwa sana Kwa Kumfix Rais Samia kwa sehemu ya upande wa Kumshughulia Mbowe Pili Kwa Rais Kukosa taarifa Muhimu za Kesi ilikuwa ni ishara kwamba alipewa Sumu na Kujazwa Chuki dhido ya Mbowe kwa Jambo asilolifahamu
Hata hivyo Mahojiano yale yalikuwa na Faida Kubwa sana Kwa upande wa Mbowe na Wenzake Watu wengi wenye mapenzi Mema na Rais Samia walijitosa Kumuokoa na Matope yale kwa Kumshawishi na Kumbeleleza aachane na Kesi ile ambayo waliona ilikuwa inamuharibia kisiasa
Mahojiano ya Rais Samia na BBC ndiyo yalizaa Makundi Mengine ambayo yalijitosa Kupamban ana kundi la Mfumo na Dola lililotengeneza Mradi wa Kumsulubu Mbowe 1.Viongozi wa CCM wastaafu 2.Viongozi Wa Serikali ya Sasa 3.Viongozi wa Dini 4.jumuiya za Kimataifa 5.Wafanyabiashara pia
Wote hao walikuwa wanamsaidia na Kumpigania Rais Samia mwenyewe wala siyo Mbowe Wao waliamini Rais kadanganywa na Kupotoshwa na Watu wake Ndiyo maana Rais Samia ktk Mahojiano na BBC Taarifa za mfumo walizompatia alijua ktk kesi ya Mbowe wapo waliohukumiwa tayari wakati si kweli
Tarehe 13 August 2021 Serikali na Magereza waliendeleza Vituko na Visa vyao Kwa kushindwa Kumleta Mbowe na Wenzake Siku ya Kesi kwa Kisingizio cha Gari ya Magereza iliyotakiwa Kumleta Mbowe ilikuwa mbovu Walishindwa tena Kuunganisha Mtandao wa Video ya Gerezani na Mahakamani
Siku ya Ijumaa ya Tarehe 13 August 2021 Kesi ya Mbowe ilihairishwa hadi tarehe 27 August 2021 Mawakili wa Mbowe wakimlalamikia Hakimu kutaka atoe tamko rasmi la kuwataka Magereza Kuhakikisha Wanamfikisha Mbowe Siku hiyo Hakimu Simba Kwa tabu sana na Shingo upande akatoa tamko
Lakini kwakuwa Presha ilikuwa Kubwa ndani na nje ya Nchi kesi haikusubiri tarehe 27 August 2021 kama ilivyo kuwa imepangwa na Mahakama hapo Mwanzo Mawakili wa Mbowe walipokea Mwaliko wa Mahakama tarehe 20 August 2021 Siku ya Ijumaa kuwa Jumatatu 23 August 2021 kesi itaendelea
Jumatatu ya 23 August 2021 Serikali ilikuwa imekamilisha nyaraka zote kwa ajili ya kupeleka Mahakama yenye mamlaka ya Kusikikiza kesi ile Pale Washitakiwa wote Walisomewa Maelezo ya COMMITTAL na hawakutakiwa Kujibu lolote Serikali ilikuwa imeandaa Mashahidi 24 na Vidhibiti 19
Kesi ilihairishwa na Siku hiyo ya Tarehe 23 August 2021 ndiyo ikawa mwisho wa Kesi ya Mbowe Kuitwa Mahakama ya Kisutu Mawakili wa Mbowe Wakawa sasa Wanasubiri kesi Kuitwa Mahakama kuu baada ya Kujulishwa ni lini na mbele ya Jaji gani...!
ONA JINSI WATU WA USALAMA (MFUMO) NA DOLA WALIVYO CHEZEA KESI YA MBOWE PALE MAHAKAMA YA KISUTU. ipo hivi kabla ya Mwenyekiti Mbowe Kukamatwa na Kushitakiwa Siku ya tarehe 26 July 2021 Wenzake alioshitakiwa naye walikamatwa na Kushitakiwa yangu tarehe 19 August 2020
Kesi hiyo iliitwa Kesi ya Uhujumu uchumi namba 63 ya Mwaka 2020 Ilikuwa na Watuhumiwa watatu tuh ambao ni 1.Khalifan Bwire 2.Adam Hassan Kasekwa 3.Mohammed Adbillah Ling'wenya Ilisimamiwa na Mawakili Wa serikali waandamizi wawili 1.Shadrack Kimaro 2.Wankyo Simon
Wakati huo Kesi ilikuwa haina ishu wala haina Mvuto ingawa ni Ukweli walikamatw Walinzi wa Mwenyekiti Mbowe na Mawakili wa Chadema walikuwa wanaisimamia Kesi ilikuwa Mbele ya Hakimu Mkazi Simba wa Kisutu Lakini ilipofika tarehe 8 Sept 2020 Serikali iliongeza Mtuhumiwa mmoja
Na ilipofika tarehe 30 September 2020 Serikali pia iliongeza Watuhumiwa wengine Wawili na Kufanya Jumla ya Watuhumiwa kufikia Idadi ya Watu 6
Kutoka Tarehe 30 September 2020 hadi Tarehe 26 July 2021 Kesi namba 63 ya 2020 ilikuwa imeshaitwa mara 26 kwa ajiki ya Kutajwa na Kuhairishwa Huku Mawakili wa Serikali wakisema Kuwa Upelelezi bado haujakamilika.
Lakini baada ya mfumo na Dola kuchukua Usukani na Kuendesha gurudumu la Sinema dhidi ya Kumtia hatiani Freeman Mbowe siku ya tarehe 21 July 2021 kule Mwanza Cha Kwanza wakalikamata Faili la Kesi ya Mbowe na Kuamza Kuliemdesha wao badaka ya DPP na Mawakili wa Serikali
WATU WA MFUMO NA DOLA WALIPANIA ILA HAWAKUWA SMART au WALIKUWA NA UWEZO MDOGO 1. Waliitelekeza Kesi kwa Muda mrefu na hata Hakimu simba alikuwa imetoka Mikononi mwake kwa Muda mrefu 2.Kesi kabla ya Mbowe mara ya Mwisho ilikuwa chini ya Hakimu A.Luambano wa Mahakama ya Kisitu
Hakimu A.Luambano mara ya Mwisho akiwaita Watuhumiwa sita wa Kesi ya Uhujumu uchumi namba 63 ya 2020 Siku ya tarehe 22 July 2021 na Siku iliyo kesi ilikuja kwa ajili ya Kutajwa tuh,upelelezi ulikuwa haujakamilika Na Hakimu Luambano alihairisha kesi hadi tarehe 05 August 2021
Siku hiyo Kesi iliendeshwa kwa Mtindo wa Mtandao wa Video kutoka Magerezani na Mahakamani na Serikali Waliwakikishwa na Wakili Neema Mushi
Ghafla Kesi Ikaitwa tarehe ambayo haikupangwa tarehe 26 July 2021 badala ile tarehe iliyopangwa na Mahakama ya 06 August 2021 Siku hiyo Mawakili wa Serikali 1.Esther Martin na 2.Tulimanywa Majigo Cha ajabu siku hiyo Watuhumiwa wote sita hawakuwepo Mahakamani πŸ˜‚πŸ˜‚
Na ajabu la Pili Mawakili wa Washitakiwa Sita pia hawataarifiwa kuwa Kesi imeitwa siku hiyo ya tarehe 26 July 2021 Kifupi kilikuwa Kikao cha Hakimu na Mawakili wa Serikali Wakili Esther Martin siku hiyo alimuomba Hakimu Simba ambaye hakuwa na kesi hiyo kwa zaidi ya Mwezi 1
Ombi la Kwanza la Wakili wa Serikali Esther Martin lilikuwa 1.Kuomba Kumuongeza Mtuhumiwa Mpya FREEMAN MBOWE 2.Kuwafutia Mashitaka Watuhumiwa watatu Hakimu Simba akakubaliana na Maombi yote mawili siku hiyo Kama yalivyo Ombwa
Siku hiyo tarehe 26 July 2021 Mchezo huu Unafanyika Ndiyo siku ambayo Jeshi la Polisi lilimtorosha Freeman Mbowe kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay na Kumfikisha Mahakama ya Kisutu bila Wakili wala Ndugu yoyote wa Mbowe Kujua Mbowe alisomewa Mashitaka chapchap na Kupelekwa Jela
Walishafanikiwa Jambo lao kwa Mbwembwe wakatoa Removal Order kwa Washitakiwa Watatu Hawakumruhusu Mbowe Kuzungumza Chochote wakamwambia Mahakama ya Kisutu haina uwezo wa Kukusikiliza Shauri lako Mbowe macho yakamtoka kama zongombinyoπŸ˜‚ hakuamini anachomiona wakampeleka Jela
Usiku wa Tarehe 26 July 2021 baada ya Mbowe Kufikishwa Kimafia kule Gerezani alikutana na Vijana wake 5 kati ya 6 sababu Mmoja alikuwa anaishi Gereza la Ukonga tofauti na wenzake Akaongea nao na akawahaidi atapamban watatoka wote mle gerezani Hakujua wenzie wameshafutiwa kesi
Kesho yake tarehe 27 July 2021 Removal Order ya Washitakiwa watatu ilikuwa imeshakamilika Wakatolewa Washitakiwa watatu Wakabakia Mbowe na Wenzie Watatu Katika Washitakiwa Watatu Serikali ikamfanya mmoja Kuwa shahidi wa Serikali Bwana Justine Kaaya Asaidie kumtia hatiani Mbowe
Boniface Jacob

Boniface Jacob

@ExMayorUbungo
Ex-mayor @Ubungo Municipal council 2016-2020 Exmayor @Kinondoni Municipal council 2016 Jan to Nov, Ubungo councilor 2010-2010 BA.Ed UDSM alumni CHADEMA Member
Follow on Twitter
Missing some tweets in this thread? Or failed to load images or videos? You can try to .