Thread Reader
Boniface Jacob

Boniface Jacob
@ExMayorUbungo

Twitter

SOMA UZI MPYA HAPA.....PART 3 UNTOLD STORY/RELEASED 4th MARCH/UNCLASSIFIED LEO NI 4 MARCH (from part 3) MWAKA MMOJA tangu MBOWE atoke GEREZANI baada ya KUFUTIWA KESI..! KWA NINI MBOWE ALITOLEWA GEREZANI 4 MARCH............? 18 Feb 2022 Siku Dola na Mfumo walipopata Point 3.

Yeees ilikuwa Siku muhimu sana Kwa watu wa mfumo na vyombo vya Dola Walikuwa wamefanikiwa Jambo lao la Kutolewa Uamuzi wa Jaji Tiganga kwa Mbowe Kukutwa na Kesi ya kujibu yeye na Wenzake Ilikuwa ni Ushindi Mkubwa sana Kwao,hiyo 18 February 2022 Sababu katika pande mbili zote
Mechi ilikuwa kali Juu ya nani atafanikiwa kushawishi Mama na Kusikilizwa kuhusu Kesi ya Mbowe Wale wanaoona Mbowe anaonewa au Wale wanaotaka Mbowe afunzee adabu..? Upande wa Kushoto palikuwa na Wazee Wastaafu,Viongozi waandamizi awamu ya 6,Viongozi wa dini na Wafanyabiashara
Upande mwingine palikuwa na Watu wa Mfumo,Washauri wa siasa wa Rais na Wakuu wa Vyombo Vya Dola Ni dhahiri kwa Kesi ilivyokuwa inaendelea,Dunia nzima wanaifuatilia kupitia maandiko ya neno kwa neno Kutoka Mahakamani Wengi walijua hakuna Kesi ya Kujibu kutokana na mashahidi
Mpaka siku Jaji Tiganga aliposema Kwamba Tarehe 18 February 2022 atatoa Uamuzi Dhahiri watu walijua Mbowe anakwenda Kuachiwa ilikuwa sababu mrejesho wa makundi mbalimbali niliyo yataja Kila moja kwa wakati wake lilikuwa limefanya kazi 1.kumfikia Rais 2.kumshawishi Rais
Upande wa Chadema walikuwa na matumaini makubwa sana kiasi cha Siku ya hukumu ndogo ya kama Mbowe na wenzake wanakesi ya Kujibu walikuja na Magari yenye spika hadi Mahakamani,mabango na sare za Mbowe sio gaidi Bila shaka Walijua wanaondoka na Mwenyekiti wao siku hiyo
Hata Jeshi la Polisi na Magereza pia walikuwa wanajua kwa asilimia zaidi 90% siku hiyo Mbowe angeachiwa huru kwa kukosekana na Kesi ya Kujibu Tangu asubuhi Mahakamani pale palikuwa na Polisi wa Chache sana tofauti na Kawaida yao Wanachadema waliruhusiwa Kuingia ndani kirahisi
Jaji Tiganga aliiacha Dunia mdomo wazi pale alipo Sema kuwa Mbowe na wenzie wanakesi za Kujibu Mahakama ilikuwa Imejaa sana siku hiyo,kiasi cha Kwamba baada ya Uamuzi Mahakama iliangua Vilio kama Msiba wa Ghafla na Wakina Mama wengi sana wakazimia na Kutolewa nje HATUKUAMINI
Niliwatizama Washitakiwa wote wanne walikuwa Wanacheka tuh na kupungia watu lakini Moyoni nilijua Walikuwa wamechanganyikiwa kiasi wasijue wafanye nini Wakiwa kwenye Sare zao za T-shirts nyekundu kwa pamoja eneo lao la Mahakama
Ghafla askari magereza ambao waliamini wanaachiwa huru akili zikawarejea kuwa bado tunao sana na wapo chini yetu Wakasogea na Kwenda kuwazingira kuzuia watu wasiwasalimie wala wasiwasogelee Jaji alikuwa ameshotoka ktk kiti chake na kurudi ofisini,Wakina Mbowe wakatolewa nje
Lakini sisi tuliokuwa eneo Jirani na Washitakiwa,Mbowe na Wenzake tuligundua Mbowe amekasirika Sana Kicheko chake hakikukuwa cha heri ilikuwa ni Kuwadharau watu wa Mfumo na Dola kwa Mchezo wanaoucheza Alikuwa kila anapopewa pole na Kutiwa moyo asema "WACHA WANIFUNGE"
Poli wakati wanaenda ktk gari ya Magereza Kurudi gerezani Kuna katukio kadogo kalitokea kwa sisi watu wa Jirani tulikaona Wakati sasa Watuhumiwa wanatolewa Mahakamani na Kurudishwa katika gari yao Mama Mdogo wa Khalifan Bwire alimsogelea mwanae Bwire na Kumpa maneno ya faraja
Tukio ambalo askari Magereza mmoja alilizuia kwa kumpiga Kikumbo yule mama Khalifan Bwire alilizuia kwa kusogeza mkono ili kikumbo kisimfikie Mama yake mdogo Na polisi wengine walimkata Jicho sana yule mwenzao Ishara ya Kwamba amekosea "Over do" Basi siku Ikawa imeisha
Tangu siku ile February 18,2022 Mambo yalikuwa magumu sana kwa Mawakili wa Chadema Mawakili pale Mahakamani walijikomiti kwa Jaji kwamba Siku ya tarehe 04 March wangeleta Orodha ya Mashahidi 24 lakini hawakuwa radhi kutoa orodha ya Mashaidi siku ile ya 18 Feb 2022
Lakini walipoenda Kumtembelea Gerezani Mbowe walikuta msimamo wake ni tofauti na wao Aligoma kabisa mashahidi kuletwa kwa ajili ya Utetezi wao Aliwaagiza mawakili wajiandae kwa wao Washitakiwa wa nne ndiyo watatoa Ushahidi tuh. Kama Serikali inataka kuwafunga na iwafunge tuh.
Kutoka Tarehe 18 February hadi 03 March 2022 Siku moja kabla ya Kesi Mawakili walikuwa na kazi ya Kumbembeleza Mbowe akubali wamalize kesi bila hasira wala Kususia wakiamini itawasaidia katika Mahakama ya Rufaa kama kweli Mahakama ya Mafisadi na Uhujumu uchumi itawafunga
WAKIWA JELA WANASUBIRI TAREHE 4 MARCH 2022 MUNGU ANATENDA MUUJIZA KWA KINA MBOWE Ni wale askari Magereza waliogongana Kikumbo na Khalifan Bwire siku ya tarehe 18 February 2022 pale Mahakamani Sinza Siku moja katika zile wiki mbili za kusubiri wakajitetee askari wale magereza
Walijiongeza na Kugundua Kuwa Serikali inataka kuwafunga kwa hiyo heshima kwa Mbowe na Vijana wake ikapotea tofauti na ilivyokuwa Mwanzo kabla ya Kukutwa na kesi ya Kujibu Basi Bhanaaaa siku moja Jumapili Wakiwa Khalifan Bwire na Mohammed Ling'wenya wapo sehemu nyingine gerezani
Wakati wanarudi katika Chumba Chao wanapolala na Kuwake Vitu vyao Watuhumiwa wengine wakawatonya kuwa Askari Magereza walikuja kupekua Vitu vyao Na walipotazama waliona kweli Vitu vipo shaghala baghala tofauti na walivyo viacha hapo awali Wakauliza Kuna shida gani..?
Wakati Mahabusu wengine wanawasimulia Upekuzi ulivyokuwa na Kilichotokea ghafla wale Askari Magereza walikuwa wamerudi tena katika Chumba Kile Tuhuma ya kwanza ikawa katikati ya mikate yao Pamekutwa na "Risasi za Bastola" zikiwa zimefichwa Na askari wa aonyesha risasi zenyewe
Tuhuma za Pili kwamba walikuwa wanapanga kutoroka gerezani kwa Kufanya Mazoezi na kuongea na Watuhumiwa/ Mahabusu wenye kesi kubwa kubwa Wakati wanajitetea bhanaaaaa wakadondoshewa Kipigo Kikali sana cha Mikanda na Waya pamoja na Mateke na Ngumi Waligombewa na KMKM wa gerezani
Wakati huo Makazi ya Mbowe ni tofauti sana na alipokuwa anaishi Khalifan Bwire na Mohammed Ling'wenya ingawa wote walikuwa katika gereza moja Bwire na Ling'wenya waliumizwa sana kiasi cha Kuachiwa Majeraha Makubwa Sana Kila baada ya Muda Jamaa wanarudi kuwahoji kuhusu risasi
Siku ya tarehe 03 March mawakili walienda gerezani lakini hawakujua kinachoendelea Wao walikuwa wameweka nguvu yao katika Kumshawishi Mbowe akubali waendelee na kesi kwa mujibu wa njia walizopanga Mawakili wala asisusie Kutoa Ushaidi
Laini siku hiyo hiyo ya tarehe 03 March 2022 siku moja kabla ya Kesi Mchana Mbowe alipata taarifa ya mateso ya Vijana wake akaomba Kumuona Bwana Jela Bwana Jela alikuwa hafahamu jambo lolote linaloendelea Kuhusu Makomandoo wa Mbowe Kuteswa Gerezani kwake
Mbowe alimwambia Bwana Jela hawatoenda tena Mahakamani kesho yake tarehe 04 March 2022 mpaka Dunia ijue kuwa wao wanateswa na Kupigwa wakiwa ndani ya Jela Basi weeeeeeee Bwana Jela akaona kumewaka moto cha Kwanza akaitisha Uchunguzi na Kuwataarifu mabosi zake juu ya hilo
Bhasi bhanaaaaaaaa ila Alhamisi ya tarehe 03 March 2022 Mpaka jioni Gereza la Ukonga lilikuwa limejaa watu wa Dola na Mfumo kutoka Idara mbalimbali Wapo waliokuwa wanapambana Jambo liishie mlemle Gerezani na wapo waliokuwa wanapambana Jambo litoke nje kwa Wakubwa zao
Kwa Mtu wa Dola na Mfumo alikuwa na Kazi yake Maalum katika Jambo lile Wale Askari wa KMKM Jumba bovi liliwaangukia wakubwa waliowatuma kwenda kuwatia adabu Khalfan Bwire na Mohammed Ling'wenya wakawakana mchana kweupe Wakabainika,wakabananishwa wakatakiwa kutoa Maelezo
Wakakiri kwamba wao Askari Magereza ndiyo waliweka risasi katika Mikate ya Khalfan Bwire na Mohammed Ling'wenya Kisha wakawasingizia wameingia nazo gerezani. Bwana Jela akamuita Mbowe akaomba wayamalize kwakuwa Vijana wake wamekiri na Wakubwa zake wamekuja Kushughulikia tatizo
Mbowe aliporudi Katika Chumba chake cha Kondemu (chumba cha watu wanaosubiri Kunyongwa ndiyo yalikuwa Makazi ya Mbowe) VIjana wake Khalifan Bwire na Mohammed Ling'wenya walikuwa wamehamishiwa Kule na wao kutoka Mahabusu za Kawaida Basi kabla Mbowe Kufungua mdomo vijana Wakakaza
Wakamwambia SISI KESHO HATUENDI MAHAKAMANI kama unaenda utaenda Mwenyewe Boss akawaambia nitaendaje niwaache..? Kesho msimamo wetu hakuna Kwenda Mahakamani
Boniface Jacob

Boniface Jacob

@ExMayorUbungo
Ex-mayor @Ubungo Municipal council 2016-2020 Exmayor @Kinondoni Municipal council 2016 Jan to Nov, Ubungo councilor 2010-2010 BA.Ed UDSM alumni CHADEMA Member
Follow on Twitter
Missing some tweets in this thread? Or failed to load images or videos? You can try to .